| dc.description.abstract | Katika karne ya ishirini na moja, mwanamke amewekwa mbele kinyume na ilivyokuwa
wakati dunia ilikuwa imetawaliwa na ubabedume. Hali hii inasawiri mabadiliko katika
jamii. Mabadiliko haya yamemwathiri mwanamume katika jamii. Utafiti huu
ulichunguza usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya ya Chozi la Heri na Nguu za
Jadi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhalisia. Nadharia ya uhalisia inadai
kwamba, fasihi inalenga kutoa picha halisi ya jamii husika. Nadharia hii ilizuka huko
Ulaya katika karne ya kumi na tisa. Miongoni mwa wataalamu waliohusishwa na
nadharia hii ni Georg Lukacs (1972). Utafiti huu ulilenga kuchunguza jinsi mhusika wa
kiume anavyosawiriwa katika riwaya teule. Aidha, umebainisha changamoto
zinazomkabili mhusika wa kiume katika riwaya teule. Halikadhalika, utafiti huu
umeonyesha jinsi changamoto zinazomkabili mhusika wa kiume zinavyomwathiri
binafsi na jamii yake. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani ambapo riwaya ya Chozi la
Heri na Nguu za Jadi zilisomwa na kuhakikiwa. Riwaya hizi zilichanguliwa
kimakusudi. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa na kuwasilishwa kimaelezo. Utafiti
huu umeangazia masuala ya jinsia ya kiume, jambo ambalo linahusu jamii kwa jumla.
Vilevile, kutokana na utafiti huu, jamii itaweza kubaini changamoto mbalimbali
zinazoikabili jinsia ya kiume na athari ya changamoto hizo na hivyo, kuwa na uwezo
wa kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo. Halikadhalika, utafiti huu
utakuwa kichocheo na rejea muhimu kwa watafiti wa baadaye wa fasihi kuchunguza
masuala yanayohusu jinsia ya kiume. | en_US |