• Login
    View Item 
    •   MKSU Digital Repository Home
    • Projects, Theses and Dissertations
    • MKSU Masters Theses
    • MKSU Masters Theses
    • View Item
    •   MKSU Digital Repository Home
    • Projects, Theses and Dissertations
    • MKSU Masters Theses
    • MKSU Masters Theses
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    USAWIRI WA WAHUSIKA WA KIUME KATIKA RIWAYA ZA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI

    Thumbnail
    View/Open
    Thesis (1.382Mb)
    Date
    2025-11
    Author
    KIEMA AGNES MWONGELI
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Katika karne ya ishirini na moja, mwanamke amewekwa mbele kinyume na ilivyokuwa wakati dunia ilikuwa imetawaliwa na ubabedume. Hali hii inasawiri mabadiliko katika jamii. Mabadiliko haya yamemwathiri mwanamume katika jamii. Utafiti huu ulichunguza usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya ya Chozi la Heri na Nguu za Jadi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhalisia. Nadharia ya uhalisia inadai kwamba, fasihi inalenga kutoa picha halisi ya jamii husika. Nadharia hii ilizuka huko Ulaya katika karne ya kumi na tisa. Miongoni mwa wataalamu waliohusishwa na nadharia hii ni Georg Lukacs (1972). Utafiti huu ulilenga kuchunguza jinsi mhusika wa kiume anavyosawiriwa katika riwaya teule. Aidha, umebainisha changamoto zinazomkabili mhusika wa kiume katika riwaya teule. Halikadhalika, utafiti huu umeonyesha jinsi changamoto zinazomkabili mhusika wa kiume zinavyomwathiri binafsi na jamii yake. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani ambapo riwaya ya Chozi la Heri na Nguu za Jadi zilisomwa na kuhakikiwa. Riwaya hizi zilichanguliwa kimakusudi. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa na kuwasilishwa kimaelezo. Utafiti huu umeangazia masuala ya jinsia ya kiume, jambo ambalo linahusu jamii kwa jumla. Vilevile, kutokana na utafiti huu, jamii itaweza kubaini changamoto mbalimbali zinazoikabili jinsia ya kiume na athari ya changamoto hizo na hivyo, kuwa na uwezo wa kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo. Halikadhalika, utafiti huu utakuwa kichocheo na rejea muhimu kwa watafiti wa baadaye wa fasihi kuchunguza masuala yanayohusu jinsia ya kiume.
    URI
    http://ir.mksu.ac.ke/handle/123456780/20020
    Collections
    • MKSU Masters Theses [146]

    DSpace software copyright © 2002-2015  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    @mire NV
     

     

    Browse

    All of Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsBy Submit DateThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsBy Submit Date

    My Account

    LoginRegister

    DSpace software copyright © 2002-2015  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    @mire NV