Usawirishaji wa Uhusika katika riwaya za Rosa Mistika na Maisha Kitendawili
View/ Open
Date
2023-03Author
Muia, Shadrack Tete
Mutua, John
Makoti, Vifu
Metadata
Show full item recordAbstract
Makala hii inajadili usawirishaji wa uhusika katika riwaya za Rosa
Mistika na Maisha Kitendawili. Kipengele cha wahusika ni muhimu
katika kazi ya fasihi kwani hushirikiana na vipengele vingine vya
fani ili kutoa ujumbe wa kazi ya fasihi. Kwa kawaida wahusika
hujengwa kisanaa na mwandishi ili waweze kuwasilisha dhana
mbalimbali za maisha katika jamii. Kwa hivyo lengo la makala hii
ni kuchambua uwashirishaji wa wahusika wakuu katika riwaya
za Rosa Mistika ya Euphrase Kezilahabi na Maisha Kitendawili
ya John Habwe Kwa kawaida wahusika hujengwa kisanaa na
mwandishi ili waweze kuwasilisha dhana mbalimbali za maisha
katika jamii. Kipengele cha wahusika ni muhimu katika kazi ya
fasihi kwani hushirikiana na vipengele vingine vya fani ili kutoa
ujumbe wa kazi ya fasihi. Mwandishi huwajenga wahusika wake
kwa kutumia mbinu mbalimbali ili kuwatofautisha na kuiwezesha
hadhira yake kutambua sifa za mhusika fulani na kutofautisha na
mhusika mwingine katika kazi ya fasihi. Kwa hivyo lengo la makala
hii ni kubainisha mfanano wa wahusika wakuu katika riwaya za
Rosa Mistika (Euphrase Kezilahabi) na Maisha Kitendawili (John
Habwe). Ili kufikia lengo la makala hii tumeongozwa na nadharia ya
udhanaishi. Nadharia hii imetuwezesha kubainisha sifa za wahusika
wakuu kama zilivyosawiriwa na waandishi.