• Login
    View Item 
    •   MKSU Digital Repository Home
    • Conferences / Workshops / Seminars
    • Conferences
    • 2nd International Conference
    • View Item
    •   MKSU Digital Repository Home
    • Conferences / Workshops / Seminars
    • Conferences
    • 2nd International Conference
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    USAWIRI WA VIJANA KATIKA UJENZI WA JAMII MPYA KATIKA RIWAYA TEULE YA KISWAHILI

    Thumbnail
    View/Open
    Full text (124.5Kb)
    Date
    2019-04
    Author
    MWANGI, JACKSON NDUNG’U
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Katika utafiti huu, mtafiti ameonyesha nafasi ya vijana kama mawakala wa kuleta mabadiliko katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea iliyotungwa na Ken Walibora mwaka wa 2012. Hii ni kutokana na rai kwamba vijana ndiyo wengi katika jamii na wanatekeleza majukumu anuwai katika jamii.Utafiti wetu uliongozwa na Nadharia ya Uyakinifu wa kijamii ambao unajihusisha na utetezi wa wanyonge na ukombozi wao. Mtafiti amebaini kwamba vijana ni mawakala wa mabadiliko na wanaweza kuleta mchango ambao unaweza kuwafaidi wanajamii wote. Hii ni kwa sababu vijana ni wenye nguvu za mwili na maarifa ambayo wanaweza kutumia ili kuifunza jamii. Mtafiti alitumia mbinu za utafiti za maktabani na mtandaoni. Maktabani, mtafiti alisoma riwaya teule na makala tofauti kama vile tasnifu, riwaya na tamthilia zingine zinazohusiana na mada pamoja na vitabu vyenye maelezo kuhusu Nadharia ya Uyakinifu wa Kijamii. Pia, alitembelea mtandao na kuangalia masuala yanayohusiana na vijana na pia alisoma maelezo kuhusu Nadharia ya Uyakinifu wa Kijamii. Utafiti huu ulibaini kuwa vijana wanatekeleza majukumu chungu nzima katika jamii kama vile kupigana na utawala mbaya na ufisadi, kupambana na tamaduni potovu, kubadili mitazamo kuwahusu walemavu, kukabiliana na wizi wa miswada na kadhalika. Masuala haya yanadhihirisha wazi kuwa vijana wana jukumu la kipekee katika kuleta mabadiliko katika jamii.
    URI
    http://ir.mksu.ac.ke/handle/123456780/4448
    Collections
    • 2nd International Conference [101]

    DSpace software copyright © 2002-2015  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    @mire NV
     

     

    Browse

    All of Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsBy Submit DateThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsBy Submit Date

    My Account

    LoginRegister

    DSpace software copyright © 2002-2015  DuraSpace
    Contact Us | Send Feedback
    Theme by 
    @mire NV