dc.description.abstract | Makala hii inanuia kuonesha kuwa itikadi ni dhana badilifu na nyumbufu kulingana na maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiteknolojia. Itikadi ndiyo huelekeza misimamo, mielekeo na imani ya mtunzi na hivyo kuathiri mtazamo wa mwandishi kuhusu ulimwengu unaomzunguka, ambao huweza kubadilika kulingana na wakati na mahitaji ya kijamii. Katika mkabala huo makala hii inalenga kutathmini itikadi ya mtunzi katika riwaya za Dunia Yao (2006) na Mhanga Nafsi Yangu (2013) za S. A. Mohamed. Kwa kutumia riwaya hizo, makala hii inatarajia kuthibitisha kwamba, itikadi ni dhana badilifu na nyumbufu na hutangamana na jinsi mtunzi anavyobadilisha mikakati yake ili kukidhi mahitaji ya jamii lengwa kiwakati. | en_US |